Chadema Watoa Tamko Kuhusu TBC Kusitisha Matangazo ya Bunge Laivu..Kumshitaki Nape Kwa Wananchi
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrosia na Maendeleo
(CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akitoa taarifa yake kwa wanahabari
(hawapo pichani).
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema
kitapeleka hoja kwa wananchi juu ya hatua ya serikali ya kusikitisha
matangazo ya Bunge moja kwa moja (live) kwenye Televisheni ya Taifa
(TBC) kwa madai kuwa ni kulipunguzia gharama shirika hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu
amesema kufuatia kauli ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni, Sanaa na
Michezo iliyotolewa jana bungeni, atapeleka hoja kwa wananchi ili kuona
kitendo hicho kama kinakubalika ama la.
Alisema hayo leo katika Makao Makuu ya chama hicho
Kinondoni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari,
akisema kutorusha matanagzo hayo ‘live’ ni kumnyima mtanzania haki yake
ya msingi kwa kuwa matangazo hayo yanalipiwa na kodi za wananchi
wenyewe.
Alisisitiza kuwa haiwezekani kurushwa baadhi ya vipengele,
tena nyakati za usiku, muda ambao televisheni nyingi huonyesha vipindi
vya burudani na wananchi wengi pia huwa wamechoka kutokana na kazi.
Aliitaka serikali kutaja kiasi cha fedha zinazotakiwa
kurusha matangazo hayo ‘Live’ ili atakapopeleka hoja yake kwa wananchi,
wakikubali kuchangia, wajue ni kiasi gani kitatakiwa ili hata kama TBC
itakataa, wapeleke kwenye televisheni nyingine.
0 comments: