Jeshi la Polisi kikosi cha Wanamaji Lakamata Mafuta ya Wizi aina ya Diesel Katika Bandari ya Dar es Salaam
Jeshi la Polisi kitengo cha majini limekamata tani zipatazo 20 za mafuta ya Dizeli yaliyokuwa katika Jahazi lililokuwa kando ya bandari ya Dar es Salaam likijiandaa kwa safari ya kwenda Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo hicho cha polisi cha wanamaji Bwana Mboje John Kanga amesema watu watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea.
0 comments: