Jipu: Wafanyakazi 360 wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Wakamatwa Kwa Kufanyakazi Nchini Bila Kibali

Wafanyakazi
 zaidi ya 360 wa kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara, 
wamekamatwa kwa kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali vya Uhamiaji.
Kamatakamata
 hiyo imekuja baada ya agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles 
Kitwanga la kuwakamata wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi bila 
vibali.
Jana, ofisi ya Uhamiaji ya mkoa ilifanya operesheni katika kiwanda hicho, lakini haikupewa ushirikiano na uongozi.
Ofisa
 Uhamiaji wa mkoa, Zakayo Mchele alisema walifika kiwandani hapo kufanya
 ukaguzi, lakini walikosa ushirikiano kutoka kwa Meneja Mkuu 
aliyefahamika kwa jina la Vidya Digixt.
Mchele
 alisema kutokana na meneja huyo kutotoa ushirikiano, wanamshikilia ili 
kusaidiana na Uhamiaji kuwabaini wafanyakazi wanaoishi bila uhalali na 
pia watamfikisha mahakamani.
Alisema licha ya kukosa ushirikiano, wafanyakazi 117 wa kiwanda hicho walipeleka maombi ya kutaka kupewa vibali vya kazi.
Mchele
 alisema walifanya msako katika mpaka wa Kilambo na Wilaya ya Tandahimba
 na kuwakamata watu 48 raia wa Ethiopia ambao walisafirishwa kwa malori 
kutoka Kenya.
“
 Pia, tuliwakamata raia wengine wawili wa Msumbiji wakiwa na kadi za 
kupigia kura (za Tanzania) na kukamatwa siyo kwamba msako ulikuwa 
haufanyiki siku za nyuma,” alisema.
Alisema mwaka jana idadi ya watu walioingia nchini bila kibali kwa Mkoa wa Mtwara walikuwa 121.
Ofisa
 huyo alisema katika operesheni hiyo kesi zilizopelekwa mahakamani ni 36
 ambazo zilikamilika na wahusika kutiwa hatiani na kutozwa faini, huku 
wengine wakipewa adhabu ya kutumikia kifungo.

0 comments: