EWURA katika ubora wake : Yasema Nchi Inaakiba Ya Kutosha Ya Mafuta
SERIKALI
imewatoa hofu Watanzania kuhusu uwepo wa mafuta ya kutosha nchini baada
ya kuamriwa kurudishwa kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya mafuta
yenye kiwango kisichofaa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix
Ngamlagosi, alisema kuna akiba ya kutosha na hivyo watanzania wasiwe na
hofu kwani kurudishwa kwa meli hiyo hakuna athari zozote kwa upande wa
mafuta.
Alisema
ipo akiba ya mafuta ya kutosha na kwamba Ewaura inaendelea kupokea
shehena za mafuta kama kawaida na kwa kiasi kitakachoendelea kutosheleza
mahitaji ya nchi.
Aliongeza
kuwa hadi kufikia Januari 8 mwaka huu kulikuwa na kiasi cha lita
255,052,370 kwa ajili ya soko la ndani, lita milioni 143.547 kwa ajili
ya soko la nje, na lita milioni 27.875 za dizeli kwa ajili ya matumizi
ya migodi.
“Wananchi
wasiwe na hofu. Kilichofanywa na TBS hakijaathiri chochote. Kwa takwimu
hizi ni dhahiri kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta na bado
tunaendelea kupokea,” alisema Ngamlagosi.
Aidha
alisema katika kipindi cha Desemba 2015 na Januari 2016 bei za mafuta
katika soko la dunia zimeendelea kushuka na kwamba bei za mafuta katika
soko la Tanzania zilifuata mwenendo wa bei za mafuta katika soko la
dunia.
Katika
kudhibiti ubora wa mafuta, alisema Ewura inaendelea kuchukua sampuli
kwenye vituo vya mafuta, maghala makubwa ya kuhifadhi mafuta na magari
ya kubeba mafuta, lengo likiwa ni kukagua ubora wa mafuta.
0 comments: