Njaa Kali: Wakazi wa Chamwino Dodoma Wala Viwavi Jeshi Kuikabili Njaa

Wakazi
 wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakula wadudu jamii ya viwavi 
jeshi, wanaojulikana kwa jina la fumbili kutokana na njaa kali 
iliyoikumba wilaya hiyo.
Hata
 hivyo, chakula hicho huenda kikapotea wakati wowote kutokana na mvua 
kutonyesha hivyo wadudu hao, ambao huishi kwa kutegemea majani, nao 
kupotea kwa kukosa chakula.
Mbali
 na fumbili, chakula kingine ambacho kilikuwa mkombozi kwa wakazi wengi,
 hususan Tarafa ya Chilonwa, ni matunda ya zambarau ambayo nayo 
yatakwisha wakati wowote kwani msimu wake umekwisha.
Chamwino
 ni wilaya iliyoko takriban kilomita 30 kutoka mjini Dodoma, ikikadiriwa
 kuwa na watu 349,714 na mazao ya chakula yanayolimwa kwenye wilaya hiyo
 ni mtama, uwele, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, kunde, nyonyo, 
mbogamboga na choroko.
Juzi,
 Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka aliitisha kikao cha dharura cha madiwani
 wote wa jimbo hilo lenye kata 14 kujadili suala hilo na kila diwani 
aliyechangia mjadala huo, alionyesha kujuta kugombea kwa kuwa wananchi 
wanamlilia.
Madiwani hao waliweka azimio la kusafiri kwenda Ikulu, Dar es Salaam kuwasilisha kilio cha wananchi wao.
Akizunguma
 kwenye kikao hicho, Mwaka alisema hali ya wakazi wa Chilonwa ni mbaya 
kiasi hakuna matumaini hata ya kupata mlo mmoja na badala yake wengi 
wanaishi kwa uji na matunda pori na fumbili.
Mbunge
 huyo alilaani mpango wa Serikali wa kuwapa vibali wafanyabiashara 
kwenda kuchukua mahindi katika ghala la chakula la Songea kwani bei 
zinakuwa kubwa.
“Ndiyo
 maana wanyabiashara wengi walikataa kwa kuwa bei inakuwa ni kubwa 
ambayo haiwezi kurudisha hata gharama zao, kitendo hicho kimefanya 
wafanyabiashara wa kawaida kuendelea kuwaumiza wananchi, lakini hakuna 
mwenye uwezo kipindi hiki, nasema walete mahindi ya bure siyo ya kununua
 tena,” alisema Mwaka.
Mbunge
 huyo alihoji ni kwa nini Serikali isiruhusu ghala la mahindi la Kizota,
 Dodoma kutoa mahindi kwa wafanyabiashara ili bei isiwe kubwa kama 
ilivyo sasa. Alisema bei ya sasa ya Sh15,000 kwa debe la kilo 20 ni 
kubwa na wachache ndiyo wanaoweza kuimudu.
Diwani
 wa Majeleko, Mussa Omari alifika kwenye kikao hicho akiwa na fumbili 
wengi akisema aliwakamata wakati akishirikiana na wapigakura wake kupata
 kitoweo.
Hata hivyo, hakuna diwani aliyeonyesha mshangao kwani kila mmoja alisema hata kwake wanakula wadudu hao na ni jambo la kawaida.
Mussa
 alisema hali ni mbaya zaidi kwenye kata yake na tayari baadhi ya watu 
wameanza kuvimba miguu kwa kukosa chakula, huku kukiwa na taarifa za 
vifo vinavyosadikiwa kuwa vimetokana na watu kukosa lishe.
Diwani
 wa Zajilwa, Farida Maulidi alisema katika eneo lake, kuna kaya 10 
ambazo zimeelemewa zaidi na tayari kuna taarifa za vifo viwili. “Kwangu 
hali ni mbaya sana yaani naomba tuandamane kwenda hata kwa mkuu wa mkoa 
au niungane na wenzangu twendeni Ikulu tukamuone Rais. 
Mbona, pamoja na kusema hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, huku watu wanateketea na sisi tupo? Kila siku nafanya kazi ya kutafuta uji kunusuru maisha ya watu wangu,” alisema Maulid.
Mbona, pamoja na kusema hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, huku watu wanateketea na sisi tupo? Kila siku nafanya kazi ya kutafuta uji kunusuru maisha ya watu wangu,” alisema Maulid.
Ofisa
 kilimo wa wilaya hiyo, Godfrey Mnyamale alikiri kuwa hali ni mbaya 
wilayani Chamwino na kusema kama juhudi za makusudi hazitachukulia ndani
 ya wiki moja, kutakuwa na madhara makubwa.
Mnyamale
 alisema tatizo kubwa lililoikumba Chamwino ni mvua kidogo zilizonyesha 
msimu wa mwaka jana iliyosababisha watu wasivune chakula cha kutosha.
Alisema
 ili kukabiliana na njaa iliyoanza wilayani humo tangu Aprili mwaka 
jana, jumla ya tani 14,377 za mahindi zinatakiwa kwenye vijiji 107, 
lakini hadi sasa Serikali imepeleka tani 150 tu ambazo ziligawiwa katika
 vijiji 10 tena kwa idadi ndogo.
Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alisema Serikali haijalala katika kuwaza namna ya kuwasaidia.
Galawa
 alisema katika kipindi kilichopita, Chamwino ilipewa msaada wa chakula 
lakini kilikuwa hakitoshi na ndiyo sababu hakikupelekwa maeneo yote.
“Hata
 hivyo, lazima watu wajue kuwa huwezi kuomba chakula leo na ukapewa leo.
 Leo kamati ya mkoa imeshapeleka maombi taifa na juzi niliongea na 
mhusika kwamba wanalifanyia kazi,” alisema Galawa.
Kuhusu
 wafanyabiashara kulazimishwa kununua mahindi Songea badala ya Dodoma, 
alisema jambo hilo liko nje ya uwezo wake kwa kuwa wenye kuwapangia ni 
mamlaka ya chakula.
Aliwataka
 wanasiasa kuacha kukuza mambo kuwa kuna watu wamekufa kwa njaa, badala 
yake watumie muda huo kuwahamasisha wafugaji kuuza mifugo na kununua 
chakula.

0 comments: