Safi:Serikali ya ahidi kuendelea kutatua kero za wasanii
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyevaa batiki) na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage wakiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya wasanii mara baada ya kumaliza kikao na Kamati
ya wasanii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (mwenye shati la batiki)
akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki inayofuatilia
suala la malipo ya mrabaha kutokana na kazi zao Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajumbe wa Kamati ya
wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutoka kwa
vyombo vya habari na miito ya simu. Kushoto ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza leo
jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya
ambaye pia ni Kiongozi wa Kamati ya wasanii wa muziki Bw. Nickson Simon
kwa jina la kisanii Nikki wa Pili akiwasilisha hoja za kwa niaba ya
wasanii wenzake wakati wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage leo
jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sana Bibi.
Leah Kihimbi na kushoto ni msaanii Ditto.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya
ambaye pia mjumbe wa Kamati ya wasanii wa muziki akichangia mada wakati
wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na msanii mkongwe wa
muziki wa injili Bw. Cosmas Chidumule mara baada ya kumaliza kikao na
Kamati ya wasanii leo jijini Dar es Salaam.
0 comments: