Wajane Wawili Wauawa Kwa Kukatwa Mapanga Wakidaiwa Kusambaza Kipindupindu Mkoani Mbeya
Wajane
wawili wa Kitongoji cha Bulinda wilayani Kyela wameuawa kwa mapanga
wakidaiwa kusambaza ugonjwa wa kipindupindu baada ya kufiwa na waume zao
katika eneo hilo.
Waliouawa ni Geneli Kapwela (65) na Rahabu Bungulu (70) waliokuwa wakiishi peke yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema jana kuwa wajane
hao waliuawa juzi baada ya kipindupindu kuhusishwa na imani za
kishirikina.
Takwimu za mauaji toka polisi zinaonyesha karibu watu wawili wanauawa mkoani Mbeya kwa imani za kishirikina
0 comments: