Hapakaliki Zanzibar: Maalim Seif Sharif Hamad Amwandikia Barua Papa Francis Kumwomba Aingilie Kati Mzozo wa Zazibar

Makamu
 wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa 
Francis kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na 
Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa 
mbaya.
Kwa
 mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana, Maalim Seif alimwomba 
Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha 
haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.
“Ni
 wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii 
imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na 
wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu 
wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza
 kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini 
wala kabila,” ilisema barua hiyo.
Barua
 hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na 
Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya 
wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada 
ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao 
hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.
“Badala
 ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu 
uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na 
majeshi yake  kutishia watu wa upinzani,” ilisema.
“Wakati
 mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan  wa Zanzibar  mwaka  1840  
kibali cha  kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani 
yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa
 na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.
Iliongeza
 kuwa, Zanzibar  ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa 
watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu 
yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia  na Hindu na hakukuwahi kuwa na
 mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya 
dini.
Ilisema
 Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu 
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa 
ushindi wake hata muhula mmoja.

0 comments: