News:Tundu Lissu Atofautisha Tuhuma za Ufisadi za Lowassa na Profesa Muhongo

Mwanasheria
 mkuu wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu 
ametofautisha kilichomkuta Edward Lowassa kwenye sakata la Richmond na 
kilichomkuta Profesa Sospeter Muhongo kwenye sakata la Escrow bungeni.
Akiongea
 katika kipindi cha Mada moto cha Channel Ten, Lissu alieleza kuwa kwa 
kutumia ripoti za kamati za bunge zilizomhukumu Lowassa mwaka 2008 na 
ripoti za kamati ya bunge ilizomhukumu Profesa Muhongo mwaka 2014/2015 
kuna utofauti mkubwa.
Alisema
 kuwa ripoti ya Mwakyembe ilieleza kuwa Lowassa anawajibika kwa makosa 
ya watu watano wa chini yake ambao aliwataja majina na kwamba hakuna 
sehemu ilimtaja Lowassa kuhusika moja kwa moja na sakata la Richmond.
Alisema
 kuwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyokuwa chini ya 
Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe, ilieleza wazi kuwa Profesa Muhongo 
alishiriki kudanganya kuwa fedha zile hazikuwa za umma na baadaye 
ikabainishwa na kamati hiyo kuwa zilikuwa fedha za umma.
“Kwa
 mujibu wa kamati ya Mwakyembe, Lowassa aliwajibika kwa sababu ya makosa
 ya hawa watu… Sasa hayo ni ya Lowassa. Yanalingana kiasi gani na ya 
Profesa Muhongo, yanalingana kiasi gani na ya Profesa Muhongo aliyesema 
kuwa bilioni 300 na ushee zilizotolewa Benki Kuu zikagawanywa kama njugu
 ni hela binafsi.
“CAG
 akachunguza akasema kuna hela za Umma, Takukuru wakachunguza 
hawajatuletea taarifa bungeni mpaka leo. Bunge likachunguza likasema 
hizi ni fedha za umma na hawa watu wawajibike na wakawajibishwa. Kuna 
ulingano gani hapo? Na hapo nazungumzia taarifa za kamati hizi mbili za 
bunge,” alisema Lissu.

0 comments: